JINSI YA KUZUIA MIMBA ZISIZOTARAJIWA
Kuna njia nyingi za kuzuia mimba zisizojarajiwa mfano matumizi ya condom , vipandikizi na njia nyingine nyingi.
Ila leo nmewaletea njii hii ya kalenda ambayo ni asilia na rahisi lakini pia salama kama itafanyika kwa ufasaha.
Mambo ya kuzingatia katika njii hii ni kwamba unachotakiwa kufanya ni kuzijua na kuzielewa siku zako za mzunguko
( menstration circle).
Mara nyingi wasichana wengi huwa na mzunguko wa kuanzia siku 28-31.
Siku unayoingia mwezini (period) hiyo ndio siku ya kwanza kwenye mzunguko wako. Na kuanzia hapo ndo unaanza kuhesabu moja. Na wasichana wabaingia hedhi kuanzia siku 3-5. Kwahiyo siku ya 1 unayoanza hedhi mpaka siku ya 5 tangu ulipoingia hedhi haushauriwi kufanya mapenzi kwa sababu za usafi.
Baada ya hapo siku ya 6 tangu uingie hedhi mpaka ya 10 unaweza kufanya mapenzi bila kutumia kinga wala kizuizi chochote na usipate mimba
Siku ya 11 mpaka ya 18 tokea uingie mwezini , hizi hujulikana kama SIKU ZA HATARI ambazo huwa na uwezekano mkubwa wa kupata mimba, unashauriwa katika kipindi hiki unashauriwa kutokufanya mapenzi au endapo utafanya tumia kinga na vizuizi vingine vya mimba.
Baada ya hapo siku ya 19 tokea uingie mwezini mpaka siku ya 28 au mzunguko mwingine wa pili siku hizo ni salama na waweza shiriki tendo la ndoa bila kinga na bila kupata mimba.
Kama ni wapenzi msichana na mvulana mwaweza saidiana katika kusabu siku hizo za mwanamke ili kuwa na ufanisi.
Wadada wengi huwa hawazifatilii saana sasa ni nafasi yako kama kijana au mwanamume kumkumbusha mwenza wako na kumsaidia kuhesabu...mara nyingi huwa wanapenda sana wakifanyiwa hivyo.
ZUIA MIMBA ZISIZO ZA LAZIMA.
Tukutane wiki ijayo tutaendelea na njia nyingine.

Comments
Post a Comment